HEADLINES

6/recent/ticker-posts

663 WAHITIMU MAFUNZO YA KUJENGA TAIFA KIBITI


 Na Scoastica Msewa,
KIBITI.

Jumla ya Wahitimu 663 wa Mafunzo ya JKT wa kikosi  Cha jeshi 830 cha Kibiti mkoani Pwani Mafunzo ya operation miaka 60 ya muungano kuwa tayari wakati wowote watakapohitajika kwa ulinzi na usalama wa nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jacob Mkunda  Mkurugenzi wa Askari JWTZ Brigedia Abubakari Chalo  huko wilayani Kibiti mkoani Pwani wakati wa hafla ya ufungwaji Mafunzo ya jeshi operation miaka 60 na muungano amesema mafunzo hayo yamewajenga katika stadiu nyingi za maisha ikiwa ni pamoja na ukakamavu, uzalendo, nidhamu, uhodali, kujiamini, uaminifu na Moyo wa kupenda kazi hivyo wapo tayari kulitumikia taifa.
"Mafunzo haya yamewawezesha kupigana kama askari wa miguu kwahiyo vijana muwe tayari kuwa jeshi la akiba kwani likitokea hitaji la kuwatumia msisite kutumika kwaajili ya ulinzi wa taifa letu" alisema.

 Aidha Brigedia Abubakari Chalo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza vijana hao umuhimu wakatunza afya zao ili wanufaike na fursa mbalimbali za nchi.

Amesema wakatunze afya zao kwani kama walivyokuja kujiunga walipimwa na wakati watakapohitajika kwa shughuli mbalimbali watapimwa afya kwanza.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo ambae pia ndio alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo amewataka kuendeleza utii kwa Rais wa jamhuri ya muungano na kutumia vizuri kiapo walichoapa,na kutii sheria za nchi, kanuni na taratibu za nchi.


"Niwahase tu kwamba utii mliotii hapa kwamba mtaendelea kumlinda Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania utii huo tuendelee kuwa nao pamoja na tukaufanyie kazi tunapokwenda"
"Baada ya kutoka hapa mtakwenda kuwa Viongozi mbalimbali hapo baadae kama sisi tulivyo hapa Sasa utii huo wa hicho kiapo muendelee kukifanyia kazi vizuri"
"Niwahase pia kwenda kufuata kanuni, sheria, taratibu na maelekezo mengine ya nchi yatakayotolewa na Viongozi kwani sisi sote tunaishi kwa kufuata kanuni, sheria, taratibu za serikali hatujiendei tu ovyo ovyo hapana, kwenye sehemu zenu za kazi mkazingatie"
Kamanda wa kikosi hicho 830 KJ Mohamed Karuwa amesema Vijana hao wamepatiwa ujuzi wa fani mbalimbali ikiwemo umoja na mshikamano ambayo imewaondolea tofauti ambazo walikuja nazo kama za kikabila, kidini, itikadi, kipato na mambo mengine.

Alisema pia Vijana hao wamejifunza maarifa mbalimbali katika stadi za kazi na stadi za maisha na kupenda kufanya kazi bila kuchoka wala kujali mazingira iwe jua iwe mvua kazi itafanyika.
"Tumewapa mafunzo ya awali ya kijeshi ili wawe tayari kwa ulinzi pindi watakapohitajika kwani watawekwa kuwa ni nguvu ya akiba au jeshi la akiba"
Amesema mafunzo hayo ni.kuhimu kwaajili ya kuandaa Viongozi waadilifu, wazalendo watakao litumikia taifa Sasa na baadae. 

Hawa Khamisi akisoma risala ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa amesema katika kipindi cha miezi minne wamepata mafunzo ya kijeshi kwa nadhalia na vitendo yaliyowajengea kupenda kazi na kuzingatia muda katika utendaji kazi wao.
"Kwani katika mafunzo haya tumebadili fikra zetu kuwa na mtazamo chanya na kujitambua zaidi, kujithamini na kutamvua nafasi ya Vijana katika kuchochea maendeleo ya nchi"

Post a Comment

0 Comments