HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUNUNUA UMEME KWA AJILI YA MIKOA YA KASKAZINI


 Na AMEDEUS SOMI,
KILIMANJARO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kununua umeme nje ya nchi maalum kwa ajili ya Mikoa ya Kaskazini na wapo katika hatua za mwisho katika kusaini mikataba ya ununuzi huo.

Rais samia amesema umeme huo utasambazwa katika vijiji vya mikoa yote kwa ajili ya kupanua shughuli za kiuchumi.
"Tupo kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe kanda ya kaskazini na wananchi wafaidi na umeme kwahiyo tutakua na umeme wa uhakika maji ya uhakika kila pahali, vijiji vyote vina umeme tunakwenda vitongoji na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"

Aidha Rais Samia amemweleza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuharakisha kuunganishia wananchi huduma ya maji ili fedha za mkopo wa mradi huo zipatikane.

"Ni Vijiji vinne tu vilivyounganishiwa maji hadi sasa, nikutake Waziri wa maji kuhakikisha kuwa vijiji vingine kumi vilivyosalia vinaingizwa kwenye mpango wa kuunganishwa maji tena kwa haraka"

Kisha Rais Samia akazungumzia kuhusu fedha za mradi huo akimtaka Waziri kuunganishia wananchi huduma hiyo ili fedha hizo za mkopo zipatikane.

"Mkaunganishe maji kwa Wananchi kwa Speed ya haraka muende hadaka kwenye kuunganisha maji kwa sababu fedha zilizojenga mradi huu ni fedha za mkopo kama wenyewe walivyosema hapa, hatukugaiwa ni mkopo na biashara ya maji ili ifanyike kwa vizuri na fedha zikisanywe lazima wananchi wengi waunge maji, waunge maji watumie maji fedha zikisanywe tupate kurudisha mkopo huo.

Ametoa Rai kwa Waziri kutafuta mita ambazo zitakazukiwa rafiki kwa wananchi ambazo hazitawabambikia madeni.

Post a Comment

0 Comments