HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MRADI WA MWANGA- SAME-KOROGWE WAGHARIMU ZAIDI YA BILLIONI 400 KUNUFAISHA WATI ZAIDI YA LAKI NNE


Na AMEDEUS SOMI,
KILIMANJARO.

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Machi 09, 2025, amezindua mradi mkubwa wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe uliopo Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro. Mradi huo ambao ulikwama kwa takribani miaka 19, sasa umekamilika. Mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha Lita Millioni 6 kwa siku na utanufaisha katika Vijiji 38 vya Wilaya za Mwanga, Same na Korogwe.

Mradi huo umejengwa kwenye mkondo wa chini wa Bwawa la Kufua Umeme la Nyumba ya Mungu lililopo Wilaya ya Mwanga, na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya watu 400,000 (Laki Nne) pamoja na mifugo. Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Billioni 406.07. Kwa ushirikiano wa Serikali na Wafadhili kwa upatikanaji wa fedha hizo.



Post a Comment

0 Comments