HEADLINES

6/recent/ticker-posts

KEDS YATOA ZAWADI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA WANAWAKE WA JIRANI NA KIWANDA

 Na Scolastica Msewa,
PWANI.

Katika  muendelezo  kusherehekea Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani Kiwanda Cha Keds Tanzania Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani  Pwani kimetoa zawadi ya bidhaa zinazozalishwa Kiwandani hapo kwa Wanawake wanaoishi maeneo ya kuzunguka kiwanda hicho.

Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi hizo za sabuni ya unga 15 na za miche katuni 10 kwa kina mama 89 wanaoishi  katika eneo jirani na Kiwanda hicho kilichopo Kata ya Picha yandege Kibaha mkoani Pwani..

Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Keds Tanzania Limited  Bob Chen  amesema   kuwa wametoa zawadi hizo kwa akinamama ikiwa ni katika kuwatakia kila lenye kheri wanawake wote  na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wakazi hao utakapohitajika.

Cheng amesema kuwa wamewapatia misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa wanawake ambao ni mkubwa katika kuleta maendeleo kwenye jamii.

"Kiwanda kinaungana na wanawake katika maadhimisho haya hivyo tumeona turudishe kwa jamii ikiwa ni katika ushirikiano na wananchi katika kuleta maendeleo,"amesema Cheng.

Amesema kuwa kiwanda kitaendelea kushirikiana na jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hususani kwa wananchi walio jirani na kiwanda na wananchi wote kwa ujumla.

Meneja wa Keds Michael Mbaraka Lugalela  amesema kuwa utaratibu huo  wa  kutoa  zawadi kwa wananchi  utakuwa endelevu kwa jamii.

Akishukuru kwa msaada huo wa sabuni za unga na vipande Jasmini Issa amesema kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani utawasaidia katika matumizi ya kila siku.

Issa amesema kuwa msaada huo umeonyesha jinsi kiwanda hicho kinavyoshirikiana na jamii katika suala zima la maendeleo ambapo wamekuwa wakisaidia miradi mbalimbali inayohusu wananchi.

Naye Meri Mkwizu amesema kuwa sabuni ni muhimu sana kwa familia na ni moja ya vitu muhimu katika mahitaji kwenye familia na hutumika muda wote.

Mkwizu amesema kuwa sabuni ina bajeti kubwa kutokana na matumizi yake ikiwa ni pamoja na kufulia nguo, kuoshea vyombo, kuogea na kufanyia usafi wa aina mbalimbali ambapo jumla ya wanawake 89 walipewa msaada huo.

Post a Comment

0 Comments