Na Scolastica Msewa,
KIBITI, PWANI.
Wananchi Wilayani Kibiti Mkoani Pwani Wametakiwa kuilinda vyema miradi ya maji ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA waliyojengewa na Serikali Ili iweze Kudumu na kuwanufaisha wengine na kuwa endelevu kwa kuitumia vizazi na vizazi.
Wito huo umetolewa na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kibiti Wakati wa Ziara ya kukagua miradi ya maji ya RUWASA ikiwamo mradi wa visima 900 vya Mama Katika vijiji mbalimbali.
Kamati hiyo ikiomgozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Juma Ndaruke amesema Kwa hatua hiyo ya miradi waliyoitembelea amempongeza maneja na jopo lake Kwa usimamjzi mzuri na kumtaka kuendelea kukamilisha miradi iliyobaki Ili Wananchi waweze kuendelea kunufaika na upatikanaji wa maji Kwa urahisi na wepesi zaidi.
Aidha naye Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kanali Joseph Kolombo amesema miradi hiyo ni mkombozi Kwa Wananchi na hapa na yeye akiwa ni Mkuu wa usalama wa Wilaya atahakikisha miradi hiyo inalindwa Wakati Wote Ili kuweza kusaidia vizazi vijavyo.
Meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Wilaya ya Kibiti Ramadhani Mabula ameeleza namna miradi hiyo ilivyotekelezwa mpaka kufikia miradi hiyo Baadhi kuanza Kutoa maji Hali inayowafanya Wananchi kufurahia huduma hiyo ya maji.
Nao Baadhi ya Wananchi waliofika Katika miradi hiyo wamesema awali walikuwa wakipata maji Katika visima ambayo si Rafiki na walikuwa wakidamka Ili kuweza kupata maji Hayo Lakini Kwa Sasa Hali ni tofauti wanatumia maji safi na salama ambayo yanaoatikana Kwa Wakati na nei nafu ikikinganisha na KIPINDI Cha Nyuma walikuwa wakinunua maji dumu sh mianane na saizi wananua sh hamsini Kwa ndoo.
Kamati ya Siasa imetembelea miradi Katika vijiji vya Pagae, Nyakaumbanga, mlanzi, jaribu mpakani, Mjawa, Nyanjati ambapo Ziara hiyo ilitanguliwa na zoezi la upandaji miti Ili kuweza kuendelea KULINDA mazingira.
0 Comments