HEADLINES

6/recent/ticker-posts

FUTARI, NYAMA CHOMA, KUNOGESHA USIKU WA KUKIKARIBISHA KILELE SIKU YA WANAWAKE ARUSHA.


Na Mwandishi Wetu,
ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kwenye "Usiku wa nyama choma" unaofanyika leo Machi 07, 2025 kwenye barabara za kuzunguka mnara wa saa maarufu kama Clock tower kuanzia majira ya saa kumi na mbili za jioni.
"Ni utamaduni wetu kula nyama na hapa tulipo ni sehemu ambayo nyama italika leo Jioni. Kwakuwa mkoa wetu una waumini wa dini zote mbili, wakristo na waislamu, na wengi tupo kwenye mfungo wa Ramadhan na Kwaresma, kwahiyo nyama hizi zitaanza kuliwa jioni baada ya futari na nyama hizi zote hazitauzwa hata pingili moja,nyama zote ni bure kwaajili ya wananchi wa Mkoa wag Arusha ikiwa ni kuashiria kwenda kwenye kilele cha siku ya wanawake." Amesema Makonda.

Akizungumza na wanahabari wakati akikagua maandalizi ya shughuli hiyo, Mhe. Makonda ametaarifu kuwa nyama choma hizo ni kwaajili ya wananchi wote wa Mkoa wa Arusha na zimeandaliwa na kutolewa bure kwa kuwezeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kudhihirisha mapenzi mema kwa wananchi wa Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania.

"Nyama hizi tunasema ni bure kwa wewe mwananchi unayekuja kula lakini Dkt. Samia ndiye aliyegharamia kuhakikisha zinawafikia wananchi wa mkoa wa Arusha na kuendeleza utamaduni wao wa kula na kufurahi pamoja."

 

Post a Comment

0 Comments