Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo Waziri amesema Ushiriki wa akina mama katika biashara utasaidia zaidi katika uchumi wa nchi kwani zaidi ya asilimia sabini za biashara ndogondogo zinafanywa na akinamama.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake kunufaika na Soko huru la Afrika Waziri Jafo amesema Wizara ya Viwanda na Biashara itasaidia kuondoa vikwazo vya kikodi baina ya nchi ili kisaidia uwezeshaji wa biashara.
Amewaasa Chemba ya wafanyabiashara wanawake (TWCC) programu ya kusadia wanawake kibiashara ifikie katika maeneo mengi zaidi ili wanufaike na kujikwamua kibiashara ili kuongeza pato la Taifa.
Kwa upande wake Rais wa TWCC CPA Mercy Sila amesema programu hiyo ina lengo la kusaidia kuboresha uelewa wa wanawake na vijana wa mfano 50 kuhusu kanuni za biashara za mipakani, fursa na mbinu bora ili kuwasaidia kufanikiwa katika masoko kimataifa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema licha ya mafanikio zipo changamoto zinazowakabili ikiwemo wanawake na vijana kukosa mitaji ukosefu wa maarifa ya biashara na upatikanaji wa masoko.
Mwajuma amefafanua biashara 50 zitakazopigiwa mfano ni zile za sekta ya madini, viungo, nguo na mengineyo.
Chemba ya wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwa udhamini wa Trademark Africa imezindua Programu ya kuwawezesha wanawake kunufaika na ufanyaji wa biashara katika soko huru la Afrika (AfCFTA) itakayojulikana kama "Twende Sokoni Afrika".
0 Comments