Na AMEDEUS SOMI ,
DODOMA.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiwa pamoja na baadhi ya viongozi na Watendaji wa Serikali wakitazama eneo ambalo uwanja wa mpira wa miguu Dodoma utajengwa muda mchache kabla ya shughuli ya Utiaji Saini kati ya Wizara hiyo na Kampuni ya Lemonta SPA mapema leo Februari 13, 2025.
Ujenzi huo unatarajiwa kuisha baada ya miezi 24 na utagharimu shilingi Bilioni 352 hadi kukamilika kwake.
Uwanja wa Michezo unaotarajiwa kujengwa jijini Dodoma utagharimu shilingi Bilioni 352 ambazo ni fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Prof. Kabudi amesema hayo leo Februari 13, 2025 jijini Dodoma wakati wa hafla ya Utiaji Saini kati ya Wizara hiyo chini ya Katibu Mkuu wake Ndg. Gerson Msigwa na Kampuni ya Limonta SPA kutoka nchini Italia.
Prof. Kabudi ameeleza kuwa, ujenzi wa uwanja huo utatumia muda wa miezi 24 na utakuwa na uwezo wa kubeba watu 32,000.
Aidha, Waziri Kabudi amesema kuwa Serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu mingine ya michezo kama vile ukarabati wa Uwanja wa Mkapa ambao umefikia asilimia 75 na uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa uwanja wa Michezo unaotarajiwa kujengwa jijini Dodoma utagharimu shilingi Bilioni 352 ambazo ni fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Prof. Kabudi ameyasema hayo leo Februari 13, 2025 jijini Dodoma wakati wa hafla ya Utiaji Saini kati ya Wizara hiyo chini ya Katibu Mkuu wake Ndg. Gerson Msigwa na Kampuni ya Lemonta SPA kutoka nchini Italia.
Kabudi ameeleza kuwa, ujenzi wa uwanja huo utatumia muda wa miezi 24 na utakuwa na uwezo wa kubeba watu 32,000.
0 Comments