Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Godlisten Malisa ametaja mambo sita yatakayokiokoa Chama hicho kitumbukie shimoni mara baada ya Uchaguzi.
Malisa ametaja mambo hayo leo Jumapili Januari 12, 2025 katika mkutano na Waandishi wa habari
Mambo hayo ni :-
"1. Sekretariati iwakumbushe wagombea kanuni za uchaguzi zinazuia wagombea na wapambe wao kutoa lugha chafu "ni album viongozi wanawadhalilisha viongozi wenzao na wamelala na Katiba"
"2. Hatua za kinidhamu zichukuliwe kama uongozi wa Kanda ya Serengeti dhidi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga"
"3. Wagombea na wapambe wao wakumbuke huu ni uchaguzi ndani ya chama sio vita wanaweza kushinda bila kukashifiana"
"4. Uchaguzi wa ndani ufanyike baada ya uchaguzi Mkuu ili kuondoa nafasi ya watu wanaoweza kukimbia chama wakihisi wameonewa na kwamba muda huo ni mfupi wa kutiba majeraha"
"5. Kuundwe kamati Maalum ya kutibu majeraha yaliyotokana na kampeni hizi na hapa tunaweza kuwatumia viongozi wa dini na wazee wa chama"
"6. Wagombea washikane mikono na wakubaliane ili kuondoa mpasuko utakaosababishwa na uchaguzi" - Godlisten Malisa, Mwanachama wa CHADEMA
0 Comments