Na Mwandishi Wetu.
Kibiti, PWANI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Hanan Bafagih amekutana na Wakuu wa Shule za Sekondari za Wilaya hiyo kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo katika majukumu yao ya kila siku.
Wakuu hao wa Shule wameitoa kero zao mbele ya Mkurugenzi huyo wakisema changamoto zinazowakabili ni pamoja na kutolipwa stahiki za uhamisho na likizo kwa wakati, mifumo ya utekelezaji wa miradi kuchelewa, utoro wa wanafunzi, upungufu wa walimu, jamii kutokuwa na utayari wa watoto wao kusoma, uhaba wa samani, umeme na maji kwa baadhi ya shule.

“Naomba muwe na uvumilivu watumishi kufanya kazi kwa upendo, kujiamini, kuheshimiana, kushirikiana na kuvumiliana katika utendaji sambamba na kuwa na subira katika mambo yao wakati yanafanyiwa kazi.
"Kwa changamoto yeyote Ofisi yangu iko wazi , ikiwezekana tengenezeni utaratibu wa kuwasilisha changamoto zenu kwangu moja kwa moja” Amesema Bafagih
0 Comments