HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TANZANIA KUWEKEZA NGUVU KUWANIA TENA NAFASI YA WHO


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaweka kila aina ya nguvu kwa Watanzania wabobezi ili kushiriki katika nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika baada ya Dkt. Faustine Ndugulile  aliyekua mteule wa nafasi hiyo kufariki dunia.
"Tutaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ile, tutatafuta Mtanzania mwenye sifa zinazoweza kushindana na Ulimwengu, tutaingia tena na tutaweka nguvu ile ile ili kuweka heshima ya nchi yetu".
Rais wa Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na waombolezaji kabla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Marehemu Faustine Engelbert Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Faustine Ndugulile (Picha na Ikulu Tanzania)



Post a Comment

0 Comments