Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa kwa mafanikio makubwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 80 katika Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo katika Ziwa Nyasa Mkoani Ruvuma, unaotarajiwa kukamilika 2026.
Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua umuhimu wa kujengwa kwa Bandari ya kisasa katika Bandari ya Mbamba Bay.
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) imesema, Bandari ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa Mkoani Ruvuma ni muhimu katika Maendeleo ya Kiuchumi, itafungua biashara katika nchi za Malawi, Zambia pamoja na Msumbiji katika usafirishaji wa mizigo ya makaa ya mawe pamoja na mazao katika Mikoa inayoizunguka ziwa hilo.
Akizungumza katika ziara ya Bodi hiyo kwenye Bandari ya Mbamba Bay Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia amesema, Bandari hiyo itakuwa na huduma zote, TASAC wadhibiti na wasimamizi wa vyombo vya Usafiri majini watahakikisha usalama unazingatiwa na kwamba, Bandari hiyo zamani ilikuwa na changamoto ya Barabara lakini suala hilo Serikali ya Dkt. Samia ilishakamilisha kwa asilimia 100.
Mhandisi Mkuu Bandari za Ziwa Nyasa Fabian Paul anaeleza hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo wa kimkakati kwa nchi, ambapo amesema kuwa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia tisa na kufikia hapo kulitokana kuchelewa kwa vifaa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri amesema bandari hiyo inafungua milango kwa Wawekezaji wa Sekta mbalimbali huku wananchi wa Wilaya ya Nyasa wakiamini kuwa, kukamilika kwa Bandari hiyo kwao ni fursa.
#KAZIINAONGEA
0 Comments