HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASIMAMISHA UCHIMBAJI MADINI KWENYE MTO ZILA KIJIJI CHA IFUMBO, MKOANI MBEYA


Na Mwandishi Wetu,
MBEYA. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesimamisha shughuli za uchimbaji zilizokuwa zikifanywa na kampuni ya G & I Tech Mining Company Ltd kwa kipindi hiki cha mvua za masika mpaka pale tathmini ya kitaalamu ya mazingira itapokamilika juu ya shughuli za uchimbaji madini kwenye Mto Zila ili kuepusha uharibifu wa mazingira.

Uamuzi huo wa Serikali umekuja kufuatia agizo la Rais Samia, la kuona shughuli zote za Kiuchumi hususan za madini zinafanyika kwa utulivu bila kuleta migogoro na pasipo kuathiri mazingira ya eneo shughuli zinapofanyika.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde ametoa maagizo hayo 30 Disemba, 2024, katika kijiji cha Ifumbo, Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya, alipotembelea eneo la leseni ya Mwekezaji ambalo lilivamiwa na Wananchi, na kusababisha mgogoro mkubwa na uharibifu wa mali za Mwekezaji huyo.

"Tumetembelea maeneo yote mawili, na sote tumejionea hali halisi ya mazingira, ni dhamira na maelekezo ya Rais Samia kuona shughuli zote za kiuchumi hususan za madini pasipo kuathiri mazingira, na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Watalaamu wa Mazingira, Wataalamu wa Mkoa na Wananchi katika muda mfupi ujao inakwenda kuunda Timu ya pamoja ya kufanya tathmini ili itueleze kitaalamu iwapo shughuli hizi zinaweza kuendelea kufanyika pasipo athari kwenye mazingira ya Mto Zila,”amesema.

Amesema, amesikiliza hoja za Wananchi juu ya uharibifu  wa mazingira ya Mto Zila, Serikali itaunda timu ya wataalamu kufanya tathmini ya kina ya mazingira juu ya athari zinazoweza kutokea wakati wa uchimbaji wa madini na kwa sasa shughuli zote za uchimbaji madini zisimame kipindi hiki cha masika kama NEMC ilivyoelekezana amewataka Wananchi kuacha vitendo vya uvunjifu wa amani na kujichukulia sheria mkononi, na amelaani kitendo cha kuvamia na kuharibu mali za mwekezaji.

Awali, akitoa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbarak Batenga, ameshukuru ujio wa Waziri wa Madini na kusisitiza kuona mwanga utakaoleta suluhisho la kudumu katika mgogoro baina ya Mwekezaji na Wanakijiji wa Ifumbo na kwamba, Serikali ngazi ya 

Wilaya itaendelea kusimamia sheria na kanuni ili kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama muda wote.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments