Matibabu ni gharama kubwa hasa kwa watoto, kuondolewa kwa kifurushi cha Toto Afya Kadi kuliwaathiri wengi, hata hivyo usikivu wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umekuwa na tija na sasa kifurushi hicho kinarudi kwa kishindo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza kukirejesha kifurushi hicho na kinatarajia kuzinduliwa Disemba 17,2024 jijini Dodoma.
Hatua hii ni juhudi za serikali ya Rais Samia katika kuhakikisha inaboresha huduma ya Afya na kuwafikia Watanzania wote kwa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kupitia dhamira ya Bima ya Afya kwa wote.
Uzinduzi wa Mifumo hiyo unafanyika baada ya Mfuko kutekeleza agizo la Rais la kuhakikisha Mifumo ya Serikali inasomana.
Kwa upande wa Toto Afya Kadi, Mfumo umefanya marejeo ya kifurushi hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kundi la watoto chini ya umri wa miaka 18, hali ya kipato cha wananchi pamoja na hali ya Mfuko.
Kwa sasa Mfuko unaendelea na utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote hususan katika usajili wa wanachama kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kundi la wanafunzi, kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa gharama ya Shilingi 50,400.
Mfuko unatoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha kupitia mtandao mpana wa vituo zaidi ya 10,000 vya kutolea huduma nchi nzima.
#KAZIINAONGEA
0 Comments