HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA


 Na Mwandishi Wetu,

Changamoto ya uhaba wa ajira ni kubwa, vijana wengi wasomi wako mtaani wakiwa hawana ajira rasmi.

Hali hii inasababisha nchi kuwa na idadi kubwa ya vijana tegemezi wasioweza kulipa kodi kwa maendeleo yao na ya taifa kwa ujumla.

Kwa kuliona hilo Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imekuja na mpango Mkakati unaolenga kuongeza wigo wa ajira hadi kufikia ajira mpya milioni 1.2 kila mwaka. 

Tayari mpango huo umeshaanza kazi, ambapo katika kipindi cha Januari hadi Julai, 2024, tayari zimezalishwa ajira mpya  607,475 nchini.

Hatua hiyo imesaidia  kupunguza changamoto ya  uhaba wa ajira kwa wastani wa asilimia 50.6 ya lengo la uzalishaji wa ajira mpya  kwa Mwaka.

Aidha Serikali imeendelea kuweka Mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa nje na ndani ili kuboresha shughuli za uzalishaji katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji Madini, Viwanda na Biashara ili kuongeza wimbi la wawekezaji katika sekta muhimu za kimkakati.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments