HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA SAMIA INAKUJA NA MIFUMO IMARA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE


 Muda wa wananchi wa Tanzania kuendelea kutaabishwa na gharama za matibabu unaelekea ukingoni kutokana na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuandaa mifumo imara ya Bima ya Afya kwa wote.

Tayari Waziri wa Afya, Jenista Mhagama na ujumbe wake akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ismail Rumatila, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu  pamoja na wataalam wengine Disemba 09, 2024 wamefanya ziara ya mafunzo ya namna bora  mfumo wa uendeshaji wa masuala ya afya unavyofanya kazi chini ya Wizara ya Afya Uingereza.

Hatua hii ni muhimu kuelekea utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote nchini Tanzania kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mifumo imara katika usimamiaji wa huduma za afya.

"Miongoni mwa mambo tuliyojifunza kutoka kwa wenzetu wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Afya ya Uingereza Dkt. Kevin Miles ni pamoja na jinsi huduma za afya kupitia Bima ya Afya zinavyotolewa kwa wanachama, mifumo ya utoaji wa huduma kupitia Bima ya Afya jinsi inavyofanya kazi pamoja na namna ambavyo wanalipwa watoa huduma hao," amesema Waziri Mhagama.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments