Na Mwandishi Wetu,
MWANZA.
Ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, TEMESA imewezeshwa ujenzi wa Vivuko vipya sita, Vivuko saba vya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vivuko ambayo ni maegesho na majengo ya abiria katika Ziwa Victoria na Bahari ya Hindi, ambavyo gharama yake ni jumla ya Shilingi Bilioni 67.4.
Mradi huu wa Vivuko umefanikiwa kutokana na jitihada za Rais Samia, ambapo Serikali yake imetoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameongea hayo Jijini Dodoma, wakati wa mkutano wake na Wakala huyo ambapo amesema kuwa, kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 37 zimetumika kujenga vivuko sita.
Hizi fedha zote kuanzia vivuko sita vipya, vivuko saba vya ukarabati na maeneo ya maegesho, tumepata kutoka Serikali ya Rais Dkt. Samia, ndani ya miaka mitatu jumla Shilingi Bilioni 67.4.
“Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutuwezesha kufankkisha Mradi huo, na tayari zimepatikana fedha kwa ajili ya vivuko vingine saba, ambavyo jumla ya Shilingi Bilioni 20.5 ambazo zimewekezwa katika mradi huo, hili ni jambo kubwa sana,” amesema Ulega.
Waziri huyo aliutumia mkutano huo kupongeza ukarabati wa karakana za matengenezo ya magari unaoendelea kufanyika kote nchini na kusisitiza ukarabati huo uendane na mabadiliko ya kimtazamo, utaalamu na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ili kuleta tija na ufanisi katika majukumu yao.
Waziri Ulega pia ameupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA kutoka Mikoa yote nchini, kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwataka waongeze jitihada zaidi katika kazi zao.
#KAZIINAONGEA
0 Comments