Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetumia Shilingi bilioni 32 kwa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kufadhili miradi mbalimbali ya utafiti nchini kote.
Fedha hizo zimesaidia zaidi ya mipango 20 ya utafiti mahususi ya sekta, hasa katika kilimo, elimu, afya na nishati ambapo kupitia program mbalimbali zimesaidia vijana kutimiza ndoto zao
Kupitia mradi huo Serikali imeiwezesha Tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa viwango vya juu na kuifanya kuwa miongoni mwa taasisi za mfano katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
#KAZIINAONGEA
0 Comments