Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewataka Askari Polisi kuvaa sare za kazi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ili kuepuka taharuki katika jamii kufuatia kuibuka kwa matukio mfululizo ya watu kudai wanatekwa na Askari Polisi.
Hatua hii inaonyesha jinsi Serikali ya Awamu ya Sita, ya Rais Samia, inavyojali na kuthamini usalama wa Wananchi wake na kutoridhishwa na hali za taharuki zinazosababishwa na baadhi ya watu katika jamii.
Akiongea na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema, kumekuwa na maneno kwenye mitandano inayovuruga taswira ya nchi, kwa baadhi ya watu kutoweka na kudai wametekwa na baadae kubainika aidha walijificha ama wamekutwa wamefariki kwa sababu nyingine zisizohusiana na Jeshi la Polisi.
Akielezea vitendo hivyo huku akigusia baadhi ya matukio ya utekaji ambayo yametokea hivi karibuni, Chalamila amesema, mfano ni lile tukio la Mfanyabiashara Deogratius Tarimo na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo ambayo Polisi walihusishwa nayo kutokana mazingira ya matukio hayo.
“Hii tabia ya baadhi ya watu kuzua taharuki ya kuhusisha matukio ya watu kupotea na kudai wametekwa na Polisi, inachafua taswira nzima ya nchi, hivyo tumekaa na Jeshi la Polisi na kukubalina wawe wanavaa sare za kazi, pindi wanapokwenda kukamata wahalifu, ili kuzuia taharuki kwa Wananchi,” amesema Chalamila.
#KAZIINAONGEA
0 Comments