Na Mwandishi Wetu,
RUKWA.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatarajia kutumia jumla ya Shilingi Bilioni 7.4, katika ujenzi wa Soko Kuu la mazao ya nafaka eneo la Kanondo Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa, unaotarajiwa kukamilika Disemba, 2025.
Hatua hii ni muendelezo wa ujenzi na maboresho ya miradi mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia, katika jitihada za kuinua maisha ya Watanzania na uchumi wa Taifa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema, ujenzi huo wa Soko Kuu la mazao ya nafaka eneo la Kanondo, ni mkombozi wa wakulima kwani soko hilo litaongeza thamani ya mazao na kukuza mzunguko wa fedha mkoani humo.
Dkt. Dugange amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu la mazao iliyofanyika katika ukumbi wa Nazareti Manispaa ya Sumbawanga Mkaoni Rukwa, ambapo ujenzi wa soko hilo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Mradi wa Uboreshaji Miji nchini Tanzania (TACTIC).
Ujenzi wa soko hilo utajumuisha ujenzi wa eneo la kuuzia, kuandalia, kukaushia na kuchambua ili kuweka katika makundi ya ubora pamoja na eneo la maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali ya nafaka.
"Soko hili la kisasa limekuja kwa wakati sahihi kwa sababu wananchi wa Mkoa wa Rukwa ni wakulima wakubwa na wachapakazi sana, wanalisha Taifa letu, wanalisha na nchi jirani hasa kwa zao la mahindi na mazao mengine ndio maana Mhe. Rais aliona akasema lazima awaletee fedha za kujenga soko la kisasa la mazao ili tuweze kuhifadhi mazao yetu kwa ubora zaidi, tuondoe upotevu na uharibifu wa mazao unaotuletea hasara lakini pia kuongeza thamani ya mazao yetu,” amesema Dkt. Dugange.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI itahakikisha i
Amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa kwenye maeneo yote 45 yanayotekeleza miradi ya TACTIC kuhamasisha na kuelekeza wananchi kutumia vyema miradi hiyo ili kujipatia faida zaidi na kuongeza pato binafsi kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi kwenye maeneo yao.
#KAZIINAONGEA
0 Comments