HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAOKOA WANANCHI MAGU KWA UJENZI WA MADARAJA



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika kwa kupelekewa huduma muhimu katika eneo lake ikiwemo Barabara, Madaraja, Zahanati na Shule ili kila Mtanzania aweze kupata huduma muhimu za kijamii.

Katika kutekeleza azma hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa Mita 70 na Barabara unganishi ya urefu wa Kilometa 2.3.

Waziri Majaliwa amesisitiza kuwa,  Serikali ipo imara na inaendelea kuwahudumia Watanzania na kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia watanzania wote.

Katika uwekaji jiwe la msingi katika Daraja hilo uliofanyika Disemba 21, 2024 katika Kijiji cha Ngh’aya, Wilayani Magu Mkoani Mwanza, Majaliwa amesema kuwa, ujenzi unaenda vizuri na kuwahakikishia wananchi kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwa watu wa Magu na Wilaya za jirani.

“Utekelezaji wa miradi hiyo unaonesha namna Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inavyofanya kazi kwa kuleta maendeleo nchini.” amesema Waziri Majaliwa.

Mbali na kuzindua Daraja hilo, Waziri Mkuu Majaliwa, amekagua ujenzi wa Daraja la Simiyu lenye urefu wa mita 175 na Barabara unganishi yenye urefu wa Kilometa tatu.

Amesema kuwa, Serikali imeona umuhimu wa kujenga Daraja hilo ambalo lilijengwa tangu enzi za mkoloni na kuamua kulijenga upya na kuwa la kisasa.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments