HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA DKT. SAMIA YATOA MIEZI MIWILI KWA NIDA KUSAMBAZA VITAMBULISHO KWA WANANCHI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  imetoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhakikisha vitambulisho 1,200,000 (Milioni moja na laki mbili) ambavyo tayari vimeshatengenezwa, vinasambazwa na kuwafikia Wananchi.

Agizo hilo ni moja ya mikakati ya Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha kila Mtanzania aliyefikia umri wa kupata kitambulisho ya Utaifa, anapatiwa, sambamba na kufanyika kwa marekebisho kwa vitambulisho vya awali vyenye karoso ikiwemo kufutika maandishi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ametoa agizo hilo Disemba 17, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.

“Niwajibu wenu (NIDA) kuhakikisha kadi hizi mnazifutilia na zinawafikia walengwa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa", nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia Walengwa,” amesisiza Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameiagiza NIDA kuhakikisha inatengeneza vitambulisho vipya bila gharama yoyote wala usumbufu kwa baadhi ya Watanzania ambao Vitambulisho vyao vilifutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji.

Aidha, ameitaka NIDA kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuondokana na tabia ya urasimu ambapo ameiagiza Menejimenti kuanza kuwachukuliwa hatua baadhi ya Watumishi wazembe ambao hawatoi huduma nzuri kwa Watanzania.


#KAZIINAONGEA


 

Post a Comment

0 Comments