HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA AWAMU YA SITA NA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA HABARI NCHINI


 Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Habari katika kipindi cha mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yametajwa kuwa ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229, ya kuwaondolea wamiliki wa mitambo ya uchapishaji katika masuala ya kashfa na uchochezi kwa kuwa hawana uwezo wa kuingilia maudhui.

Akizungumzia mafanikio hayo wakati wa Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari, Disemba 18, 2024 Jijini Dar es Salaam, tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia, kushika nafasi hiyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa, Serikali ilikutana na wadau na kufanya marekebisho hayo.

Amesema, mabadiliko haya yamesaidia kuwaongezea uhuru Wanahabari na kuwafanya kutokuwa na hofu za kijinai kwa makosa ya kashfa na kwamba, hayo ni mafanikio makubwa katika Sekta ya Habari.

Katika mkutano huo, wadau mbalimbali waliweza kupata nafasi za kuelezea kwa ufupi changamoto katika Sekta ya Habari, ambapo wametaja kuwa ni pamoja na kuyumba kwa uchumi wa Vyombo vya Habari, Waandishi wa Habari kukosa mikataba ya ajira, Sera ya habari kuhusu uwekezaji, mafao ya uzeeni na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni miongoni mwa mambo ambayo Profesa Palamagamba Kabudi ameahidi kuyashughulikia.  

Awali akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema, licha ya mafanikio yaliyopatikana, bado kuna mapendekezo 12 waliyopeleka ya kuboresha Sheria ya Huduma za Habari hayakufanyiwa kazi.

“Mwaka jana maboresho 21 tuliyoyaomba, tisa yalikubalika yakapitishwa na Bunge, lakini 12 yalitolewa maelezo kwamba yaende kwenye Sera ya Habari ya 2003, kwa hiyo tunaamini chini ya uongozi huu mpya mapitio hayo yataharakishwa,” amesema Sungura.

Amesema, ni matumaini kwa Wanahabari kuwa, kwa kumpata Waziri Prof. Kabudi, mapendekezo hayo yatafanyiwakazi kwa haraka zaidi.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments