Katika mazingatio ya falsafa ya 4R za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita imehakikisha inaboresha huduma ya Afya na kuwafikia Watanzania wote kwa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kupitia dhamira ya Bima ya Afya kwa wote.
Aidha, katika juhudu ya serikali chini ya usimamizi wa Rais Samia, Mfumo wa Uchakataji na Kifurushi cha Toto Afya Kadi, unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, Disemba 17, 2024 jijini.
Uzinduzi wa Mifumo hiyo unafanyika baada ya Mfuko kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Mifumo ya Serikali inasomana.
Kwa upande wa Toto Afya Kadi, Mfumo umefanya marejeo ya kifurushi hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kundi la watoto chini ya umri wa miaka 18, hali ya kipato cha wananchi pamoja na hali ya Mfuko.
Kwa sasa Mfuko unaendelea na utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote hususan katika usajili wa wanachama kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kundi la wanafunzi, kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa gharama ya Shilingi 50,400.
Mfuko unatoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha kupitia mtandao mpana wa vituo zaidi ya 10,000 vya kutolea huduma nchi nzima.
Huduma kutolewa vituo zaidi ya 10,000 nchi nzima.
#KAZIINAONGEA
0 Comments