HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUFUNGA KAMERA ZAIDI YA 200 UWANJA WA MKAPA DAR

Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema Serikali ina mpango wa kuendelea na marekebisho madogo madogo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya Mashindano ya CHAN yatakayofanyika mwakani.

Marekebisho hayo ni pamoja na kufunga Kamera zaidi ya mia mbili, taa pamoja na viyoyozi ili uwanja huo uwe na muonekano wa kisasa ziadi na nakshi nzuri zitakazovutia kwani Tanzania ndio nchi mwenyeji wa Mashindano hayo pamoja na yale ya AFCON 2027 ambapo nchi itashirikiana na majirani zetu Uganda na Kenya.

Aidha Msigwa amewataka mashabiki wa soka kuacha tabia ya kung'oa viti katika viwanja mbalimbali vya michezo nchini.

Post a Comment

0 Comments