HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SAMIA INFRASTRUCTURE BOND NI RAFIKI KWA WATANZANIA WOTE


 

Na Mwandishi Wetu,

Hii hapa maana ya Samia Infrastructure Bond

1.Mtu yeyote au kundi au taasisi anaweza kununua  Samia Infrustructure Bond.

2.Kununua kiwango cha chini ni kuanzia 500,000 na kuendeleaa.

3.Bond inanunuliwa kupitia benki ya CRDB na kupitia simu yaani simbanking App kwa urahisi kabisa.

4.Kipindi cha mnada wa bond hii kitakuwa ni mwezi mmoja.

5.Riba kwa mwaka itakuwa ni asilimia 12.

6.Bond hii itaiva (mature) baada ya miaka mitano na baada ya muda huo wa  miaka mitano mtaji wa mteja utarudishwa.

7.Riba itagawiwa kila robo mwaka yaani baada ya miezi 3.

8.Bond hii haina kodi hivyo riba yako utapewa kama ilivyo bila makato yoyote.

9.Bond hii haina gharama za uendeshaji zozote kwa mteja.

10.Pesa itakayokusanywa italipa mikataba ya wakandarasi na TARURA kwa mikataba ya sasa na mipya.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments