Na Mwandishi Wetu,
MBEYA.
Juhudi za utafiti na ubunifu unaofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya MUST, zimemvutia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya kupanua huduma Mkoa wa Rukwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi alipozindua wiki ya utafiti na ubunifu katika chuo hicho.
Katika hotuba yake Mhandisi Mahundi amesema tafiti na bunifu ndiyo nguzo kuu ya uchumi Duniani.
"Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kinapaswa kuwa sehemu ya majibu na lazima wanachuo wajitofautishe na kada nyingine kwani soko la ajira kwao lipo ndani na nje ya nchi.
"Juhudi za tafiti na bunifu zenu zimemfanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuvutiwa na kutoa pesa kupanua huduma Mkoa wa Rukwa."
Aidha amepongeza Chuo hicho kwa kubuni dira za maji ambazo zinasambazwa nchini huku akihimiza bunifu zaidi katika kilimo ili waweze kujiajiri badala ya kutegemea ajira serikalini.
0 Comments