Na Mwandishi Wetu,
SONGWE.
Mwendo mrefu wa kufuata huduma za kijamii ikiwemo huduma ya afya, sasa utakuwa ni historia kwa
Wakazi wa Wilaya ya Songwe mkoani Songwe.
Tabasamu na vicheko vimetawala kwenye nyuso zao baada ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaongezea nguvu katika kujenga Hospitali kubwa ya Wilaya ya Songwe.
Wakazi wa wilaya hiyo walikuwa wanatumia muda mrefu kufikia huduma bora za afya hasa zile zinazohitaji matibabu na vipimo vya kibingwa, mwendo wa zaidi ya Kilometa tano ili kufikia huduma bora ulikuwa ni jambo la kawaida kwao.
Kwa bahati njema hilo sasa halitakuwepo kwani serikali ya Rais Samia imejenga Hospital kubwa ambayo itehudumia Wananchi wote wa Songwe na Wilaya za jirani.
Hospitali ya Wilaya ya Songwe |
Aidha Rais Samia amehakikisha Wananchi hawapati changamoto kubwa na kusafiri kwa umbali mrefu katika kupata huduma za Afya, ambapo pamoja na kujenga majengo bora, lakini pia ameongeza upatikanaji wa huduma za matibabu na vifaa tiba vya kisasa
Hii inamaanisha kazi inayofanywa na Rais Samia inaongea yenyewe kwa vitendo.
#KAZIINAONGEA
0 Comments