HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MTOTO WA MBOWE KUFUNGWA JELA ENDAPO...

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi, Januari 6, 2025  inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya waandishi wa habari Maregesi Paul na wenzake 9 wanaotaka Mkurugenzi wa Gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe aamuliwe kwenda gerezani kama mfungwa wa madai kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya misharaha yao.

Mahakama hiyo mbele ya Naibu Msaiji wa Mahakama Kuu, Mary Mrio ilitoa uamuzi huo leo asubuhi wakati shauri hilo lilipokuwa linatajwa.

Akiwakilisha wenzake Maregesi aliifahamisha Mahakama kwamba tayari hati ya wito ilishamfikia Dudley na aliahidi kufika lakini hakutokea.

Msajili Mrio alisema kwa kuwa alishapelekewa wito shauri litaendelea Januari 6 mwakani.

Waandishi hao waliamua kuwasilisha maombi ya kumkamata na kumweka gerezani Dudley ambaye ni mtoto wa Freeman Mbowe kwa sababu kashindwa kuwalipa na hata walipoingia kwenye makubaliano nje ya Mahakama Aprili 22, 2024 ya kulipa misharaha mitano hadi Mei mwaka huo hakufanya hivyo hadi leo.

Waandishi hao walishinda tuzo katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi(CMA) Julai 17, 2023 mbele ya Msuluhishi wa CMA Ilala,  Bonasia Mollel.

Madai ya awali yalikuwa jumla ya Sh milioni 114 baada ya kukaa mezani kwenye majadiliano kwa pamoja kiwango hicho cha fedha kilishuka na kufikia Sh milioni 62.7.

Dudley alikubali kulipa fedha hizo kwa awamu tatu, Oktoba 30, Desemba 30 mwaka 2023 na awamu ya mwisho ilikuwa mwishoni Februari, 2024 hakulipa na walipoingia katika makubaliano nje ya Mahakama pia kavunja makubaliano kwa kushindwa kutekeleza walichokubaliana.

Post a Comment

0 Comments