Makala fupi
Katika kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sekta ya afya imepatiwa kiasi cha Shilingi Trilion 6.722 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele mbalimbali ili kuimarisha huduma za afya nchini ambapo Wizara ya Afya imetekeleza kwa mafanikio makubwa majukumu yake, ikijikita katika maeneo Makuu mbalimbali.
Utekelezaji wa majukumu haya unatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia, kutokana na maono yake, utu na mapenzi mema ya kutaka kuona wananchi wake wanakuwa na Afya njema.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Afya imeeleza kuwa, kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha, Wizara ya Afya imeweza kutekeleza Miradi kadhaa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia ambayo ni pamoja na Miundombinu ya kutolea Huduma za Afya nchini, kuimarisha upatikanaji wa dawa na bidhaa nyingine za afya.
Upatikanaji wa huduma za Ubingwa na Ubingwa Bobezi nchini, kuimarisha huduma za Uchunguzi wa magonjwa ikiwemo huduma za Mionzi na kuimarisha Huduma za Afya ya Uzazi.
Huduma nyingine zilizoimarishwa ni huduma ya Mama na Mtoto, kudhibiti maambukizi ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa ya mlipuko, Ajira kwa Watumishi na Ufadhili wa Wanafunzi katika ngazi na fani mbalimbali pamoja na kupitishwa kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.
*Kuimarisha huduma za dharura na ajali*
Mbali na mafanikio hayo ya Sekta ya Afya katika Uongozi wa Rais Dkt. Samia, pia utekelezaji wa miradi hiyo uliwezesha kuongeza majengo ya Huduma za Dharura (EMD) kwa kukamilisha ujenzi wa majengo 23 ya kutoa huduma za dharura (EMD) katika Hospitali Maalumu za Kanda na Mikoa na kuziwekea vifaa na vifaa tiba.
Aidha kwa upande wa ngazi ya msingi, ujenzi wa majengo ya dharura (EMD) majengo 82 katika ngaziz a Halmashauri unaendelea, ambapo EMD 66 zimekamilika na zinatoa huduma.
Jitihada za Rais Samia, zimewezesha kupatikana kwa huduma za kipimo cha CT Scan zimeweza kupatikana katika Hospitali 27 kati ya Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa nchini ambapo kwa mwaka 2023, jumla ya wagonjwa 15,386 walipatiwa huduma za kipimo cha CT Scan katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, huduma ambazo hapo awali zilikuwa hazitolewi katika hospitali za Rufaa za Mikoa.
Maboresho haya katika Sekta ya Afya, yamewasaidia wananchi kupata huduma bora za tiba na vifaa tiba, kwa muda mfupi na hivyo kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania.
#KAZIINAONGEA
0 Comments