Moja ya mambo magumu kufanywa na wanasiasa wengi wa upinzani nchini ni kupongeza kitu kizuri kinachofanywa na Serikali ama Chama tawala.
Hali imekuwa tofauti kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Bila kutafuna maneno Mbowe amepongeza jitihada za maridhiano ya kisiasa zilizofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuingia madarakani.
Mbowe amesema kuwa maridhiano yalikuwa na faida kwa chama hicho na miongoni mwa faida hizo ni wanachama waliokuwa uhamishoni kurejea nchini na kufutiwa kesi zao ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe.
Ameitaja faida nyengine ya maridhiano ni kuondolewa kwa makatazo ya mikutano ya hadhara.
Maneno ya Mbowe ni jibu kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu na mashabiki wake wanaosema maridhiano ndio yamekifanya chama chao kuwa laini na kuonewa hata kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
#KAZIINAONGEA
0 Comments