Na AMEDEUS SOMI.
DAR ES SALAAM,
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) kushirikiana na Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao (MOM) Wameingia ushirikiano wa kuhamasisha kupima afya ya moyo kwa wasanii wote pamoja na wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Dkt.Peter Kisenge ametoa wito kwa wasanii wote Nchi nzima kujitokeza kupima afya ya moyo, zoezi hilo litaanza rasmi tarehe 21-DEC-2024 katika Kliniki ya moyo Kawe iliyopo Mkapa health plaza na itakuwa Bure kabisa.

"Taasisi ya moyo tumeamua kushirikiana na ninyi wote na wasanii na ndugu zetu wa BASATA ili tuweze kuwasaidia wananchi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, Mhe.Rais ametutaka kwamba tuwafikie na wasanii na watu mbalimbali kwa kuwapima kwa punguzo na tumeamua katika Kliniki yetu ambayo ipo Kawe kwa siku za Jumamosi na Jumapili tutatoa matibabu bure kwa wasanii kwa sababu afya ndio kitu cha msingi hatutaki tusikie labda msanii ameanguka akiwa anaimba".
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama ongea na Mwanao Steven Mengele amewaasa wasanii kuonesha ushirikiano katika jambo hili na kujitokeza akisema wasisubiri kuumwa ili watembeze bakuli la michango.
Mengele amesisitiza zoezi hii ni kwa wasanii wote nchi nzima na wajitokeze kupima afya ya moyo.
Vile vile amemshukuru Dkt. Peter Kisenge kwa moyo wake wa kujitoa kwa ajili ya wasanii na wananchi wote kwa ujumla.
Vile vile amemshukuru Dkt. Peter Kisenge kwa moyo wake wa kujitoa kwa ajili ya wasanii na wananchi wote kwa ujumla.
Katibu Mtendaji Basata na Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu Dkt. Kedmon Mapana kwa pamoja wametoa wito kwa wasanii kujitokeza kupima afya ya moyo.
0 Comments