HEADLINES

6/recent/ticker-posts

FORBES LAMTAJA RAIS SAMIA MWANAMKE MWENYE USHAWISHI MKUBWA DUNIANI


 Dunia inazo taasisi za kihabari zinazoheshimika kutokana na kuandika taarifa zake kwa kufanya tafiti za kitaalamu kama ilivyo kwa jarida la Forbes.

Jarida hili linaloheshimika duniani na kwa mara ya tatu mfululizo limemtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani.

Forbes wamemtaja Rais Samia kwenye nafasi ya 91 kutoka 95 aliyotajwa kwenye orodha ya mwaka 2023 ambapo amepanda kwa nafasi nne zaidi.

Mbali na hayo, Dkt. Samia anakuwa mwanamke pekee kwenye orodha hiyo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na miongoni mwa wanawake wanne pekee wanaowakilisha Afrika.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments