Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanikisha zoezi la kuandaa rasimu ya kwanza ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kupokea maoni ya takribani Watanzania 1,170,970.
Takwimu hizo zimetolewa Disemba 11,2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa rasimu ya kwanza ya Dira hiyo iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, visiwani Zanzibar.
Waziri Mkuu amemuhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kuwa Kamati ya uongozi ya maandalizi ya Dira hiyo itaendelea kufanya kazi na kutimiza majukumu yake kwa weledi, uaminifu na uadilifu ili kuleta ufanisi kwenye kuijenga Tanzania ambayo Watanzania wanaitaka kufikia mwaka 2050 huku akisema dira hiyo ni ya Wananchi.
Serikali ilikusanya maoni ya wananchi wa ndani na wale wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kwa njia mbalimbali, ikiwemo mitandao ya kijamii.
“Tulishirikiana kwa pamoja na kuhakikisha maoni ya wananchi yanatufikia kikamilifu kwakuwa Watanzania wanahitaji kuona Mpango kazi huu wa miaka mingine 25 ijayo ambayo ndiyo Dira ya Maendeleo ya Taifa,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
#KAZIINAONGEA
0 Comments