Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.
Bondia Hassan Mgaya amefariki dunia baada ya kupigwa TKO katika raundi ya sita ya pambano lililofanyika Desemba 28, 2024, ukumbi wa Dunia Ndogo, Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam.Katika pambano hilo ambalo halikuwa la ubingwa lililomkutanisha na mpinzani wake, Paulo Elias ambapo alipigwa KO raundi ya sita na mwamuzi akamhesabia.
Baada ya hesabu, alisimama na kutembea hatua chache ulingoni, kisha akaanguka na kuzimia.
Timu ya madaktari ilimpa huduma ya kwanza na kumpeleka hospitali ya Sinza kwa matibabu.
Alipofikishwa Sinza, Mgaya alipatiwa rufaa kwenda Mwananyamala, lakini alipoteza maisha kabla ya kufikishwa hospitali.
Tukio hili limezua simanzi kubwa kwa mashabiki wa masumbwi na tasnia kwa ujumla.
Cosmas Cheka, mwakilishi wa chama cha mabondia nchini, amesema wana mpango wa kumsimamisha muandaaji wa pambano, Haji Ngoswe kwa madai ya kutoshirikiana ipasavyo katika matukio yaliyohusisha kifo cha Mgaya.
Kifo cha Mgaya kimeibua maswali kuhusu usalama wa mabondia ulingoni na wajibu wa waandaaji wa mapambano.
Je, hatua gani zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda maisha ya mabondia?
Tunatoa pole kwa familia ya marehemu Hassan Mgaya, marafiki, na wadau wa masumbwi.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema.
Tufanye nini kuboresha viwango vya ulinzi na usalama kwenye michezo ya masumbwi?
0 Comments