Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Iddi Azzan Zungu amewaaasa maafisa maendeleo kuacha vitisho na mikwara kwa wakopaji wa fedha za Halmashauri akisema kuwa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaonyanyasika wakati wa ukopaji fedha hizo
Akizungumza katika Kongamano la wajasiriamali wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lililofanyika katika Uwanja wa Mnazi mmoja Naibu Spika amesema kuwa wapo baadhi ya maafisa maendeleo ambao hawafati haki katika utoaji katika utoaji wa mikopo hiyo akiwataka kufata haki.
Mbali na maafisa maendeleo pia Naibu Spika akatumia nafasi hiyo kuwataka mgambo wa Jiji waache tabia ya kuchukua rushwa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo ikiwemo mamalishe.
"Wapo baadhi ya mgambo wasio waaminifu wanachukua rushwa kwa wafanyabiashara wadogo ambao mitaji yao ni midogo unakuta mtu kwa siku hapati hata faida ya elfu mbili lakini bado mnataka kuchukua tu hata hicho kidogo"
Kazi hiyo ya kufatilia maafisa maendeleo na askari mgambo pamoja na ameitoa kwa Mkurugenzi wa Jiji kufatilia kuhakikisha mambo hayo yanafanyiwa kazi ipasavyo ikiwemo suala la kuimarisha usafi na afya za walaji au watumiaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali wa Jiji hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya |
Kongamano lilikua na lengo la kutoa elimu ya mkopo wa fedha ambapo Halmashauri ya Jiji la
Dar es Salaam inatarajia kutoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Billioni 14 na Millioni 85 kwa vikundi mbalimbali kama vile mamalishe, babalishe, maafisa usafirishaji, wajasiriamali na wadau wengine wa maendeleo ambapo jumla ya wanufaika zaidi ya 1200 wamepokea elimu hiyo
huku Taasisi ya Amo Foundation ikitoa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka safi pamoja na majiko ya gesi zaidi ya 500.
0 Comments