HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA ZAIDI YA 60 WALIOZAMIA SOUTH WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM,

Raia 64 wa Tanzania waliokuwa wamezamia nchini Afrika ya Kusini wamehukumiwa kifungo cha miezi 6 ama kulipa faini ya Tsh. Elfu 40 kwa kosa moja la kwenda Afrika ya kusini kinyume cha sheria.
Akiwasomea maelezo ya kosa, wakili wa serikali Ezekiel Kibona amesema washtakiwa kwa pamoja mnamo tarehe 29/10 /2024  Jiji la Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa wakitokea nchini Afrika ya kusini kinyume cha sheria ya nchi na hivyo akaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki amesema kuwa washtakiwa kwa pamoja wamekiri kosa lao na wameomba mahakama iwapunguzie adhabu kali kwa kuwa hawakuisumbua mahakama na hivyo akasema mahakama  inawahukumu kulipa faini ya Tsh. Elfu 40 ama kutumikia jela miezi 6.

Washtakiwa kwa pamoja baaada ya kutolewa hukumu hiyo wameshangilia huku mahakama ikiendelea wakisema maneno ya asante sana mheshimiwa hakimu. 

Washtakiwa wamefanikiwa kukidhi dhamana na wamerudi uraiani.





Post a Comment

0 Comments