Na Mwandishi Wetu,
Uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya nchi ya Tanzania na Indonesia umekuwa maradufu ikizingatiwa ongezeko la thamani ya mauzo ya nje kutoka Tanzania kwenda Indonesia kwa wastani wa Dola za Marekani Milioni 13.53 kwa 2019 hadi kufikia Dola Milioni 33.77 kwa mwaka 2023.
Ongezeko hilo limetokana na uhusiano mzuri wa Kidemokrasia baina ya nchi hizi mbili uliodumu kwa zaidi ya miaka 60 sasa,
unaendelea kudumishwa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarani.
Katika kuendelea kudumisha uhusiano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na Rais mpya wa Indonesia na Jenerali wa zamani wa jeshi la nchi hiyo Prabowo Subianto Pembezoni mwa Mkutano wa Mataifa tajiri Duniani (G20) unaoendelea nchini Brazil katika Jiji la Rio De Janeiro.
Lengo la mazunguzo ya Dkt. Samia na Rais Prabowo Subianto, ni kwa ajili ya kufahamiana na kujadili namna ya kuimarisha zaidi mahusiano ya Kidiplomasia na Kiuchumi kati ya nchi hizo mbili ambapo pia wamejadili njia za kuboresha sekta ya usafirishaji na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili.
Mwaka 2023 Tanzania na Indonesia zilisherehekea historia ya uhusiano wao, katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Tri Yogo Jatmiko, amesema mataifa hayo licha ya kuwa mbali kijiografia na kusababisha changamoto za kibiashara, lakini zina ukaribu mkubwa wa mila, tamaduni na maadili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Samwel Shelukindo ameeleza, Tanzania wanaweza kupata masoko ya biashara kupitia uwekezaji wa nchi mbalimbali ikiwemo Indonesia na kuahidi kuendeleza uhusiano huo uliodumu kwa takribani miaka 60.
Tanzania na Indonesia, zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya diplomasia, uchumi, afya na kilimo, na kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano na uhusiano wa nchi hizi umedumu maradufu ikizingatiwa ongezeko la thamani ya mauzo ya nje kutoka Tanzania kwenda Indonesia kwa wastani wa dola za Marekani milioni 13.53 mwaka 2019 hadi dola milioni 33.77 mwaka 2023.
Bidhaa kuu za Tanzania zinazouzwa nchini Indonesia ni pamoja na tumbaku, kakao, maharage, karanga, karafuu, pamba, na mafuta ya mawese.
Nchi hizi zikifanikiwa kudumisha ushirikiano huo, wakulima hapa nchini, watanufaika kwa kupata masoko ya kuuza mazao yao nchini Indonesia.
#KAZIINAONGEA
0 Comments