Na Mwandishi Wetu,
Ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya madini, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewataka watumishi wa Wizara ya Madini kuwa vinara wa kutangaza mikakati ya wizara hiyo.
Wizara ya Madini ndio kinara wa kusimamia utekelezaji wa Sera na Mipango inayoleta matokeo chanya katika sekta hiyo.
Naibu Waziri wa Madini , Dkt.Steven Kiruswa ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Madini jijini Dodoma.Ikumbukwe kuwa Sekta ya Madini ni kichwa cha Serikali hivyo kupitia Mikakati yake ukiwemo wa Vision 2030 unaosema Madini ni Maisha na Utajiri ambao una lengo la kufanya utafiti wa kina kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030 , tofauti na sasa ambapo umefanyika kwa asilimia 16.
Mkakati huo ni muhimu kwa taifa kwa sababu utawezesha kujua kiwango cha rasilimali madini na aina nyingine za madini na uwepo wa maji jambo ambalo litafungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine za kiuchumi kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Mkakati mwingine ni Mining for Brighter Tomorror (MBT) ambao unalenga kushirikisha vijana na wakina mama katika mnyororo wa thamani madini kwa kuwapatia vifaa vya uchimbaji , kuwaunganisha katika mfumo wa masoko , kuwaongezea ujuzi wa kutambua maeneo ya kuchimba kulingana na taarifa za utafiti hivyo ni wajibu wa watumishi kutangaza mikakati hii kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Kuhusu ajenda ya Nishati Safi , Dkt.Kiruswa amefafanua kuwa, Tanzania ina madini mengi ya kimkakati ambayo yanazalisha nishati safi hivyo amewataka watumishi kutumia fursa hiyo kueleza kuhusu umuhimu wa kutumia Nishati Safi ambayo ni ajenda ya kimkakati kwa Taifa.
#KAZIINAONGEA
0 Comments