HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATAKA WATAKAOCHAGULIWA SERIKALI ZA MITAA KUTUMIKIA WANANCHI


Na Mwandishi Wetu,

Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendeleza falsafa yake ya Kazi iendelee, kwa vitendo, ambapo imetoa wito kwa viongozi wa Serikali za Mitaa watakaochaguliwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi.

Novemba 27,2024 Wananchi walishiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliohusisha vyama vyote vya siasa nchini.

Akiongea kwa niaba ya Serikali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutumia vema nafasi hizo kuwaletea wananchi maendeleo.

 Ametoa wito huo mara baada ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akiongozana na mke wake Mama Mbonimpaye Mpango. 

Aidha amewataka  wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi hao katika shughuli za maendeleo watakazozisimamia.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments