HEADLINES

6/recent/ticker-posts

JAPAN YAJIVUNIA MAHUSIANO MAZURI YA KIDIPLOMASIA NA TANZANIA


 Na Mwandishi Wetu,

Balozi wa Japan Nchini Tanzania Yasushi Misawa amesema Serikali ya nchi yake imekuwa ikijivunia mahusiano thabiti na imara ya kidiplomasia kati ya  Japan na Tanzania chini ya Uongozi wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekuwa ikijiwekea mahusiano mazuri kati yake na nchi mbalimbali zilizoendelea na hii ni kutokana na ziara kadhaa zinazofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Balozi wa Japan nchini Yasushi Misawa

Katika kuisifia Tanzania, Balozi Misawa amesema, kuwepo kwa mahusiano mazuri kumesaidia kuboresha sekta za miundombinu, afya, kilimo na uvuvi kwa wananchi wa Tanzania.

Balozi Misawa ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kifupi cha utambulisho na ukaribisho kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufuatia kuwasili kwake mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Balozi Misawa amesema kuwa Japan  wanajisikia fahari kuwa sehemu ya uimarishaji wa mifumo ya utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuahidi kuwa atahakikisha anasimamia muendelezo wa uhusiano huo mwema wa kidiplomasia ambao umedumu kwa miaka mingi.

Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa iliyowahi kunufaika na mahusiano ya nchi hizi mbili kupitia miradi mikubwa inayotekelezwa kwa ushirikiano kama vile masoko ya samaki na miundombinu ya afya.

Japan ilianzisha uhusiano wa Kidemokrasia na Tanzania mara baada yakupata uhuru wake, tangu mwaka 1962 Sarikali ya Japan imetekeleza programu za maendeleo katika maeneo mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments