Na Mwandishi Wetu,
MOROGORO.
Chuo Kikuu Mzumbe, kimemtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima kwenye uongozi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Shahada hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 24,2024, Morogoro.
Mahafali hayo yamefanyika katika eneo la Mahekani, Kampasi Kuu Morogoro.
Shahada hiyo ni ya kwanza katika ngazi hiyo ya uongozi kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.
#KAZIINAONGEA
0 Comments