Na Mwandishi Wetu,
Hatimae matunda ya ziara aliyoifanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Korea Kusini yameanza kuonekana baada ya kampuni 38 kuja nchini kuwekeza.
Rais Dkt. Samia alifanya ziara hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine alikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo na kuwakaribisha Tanzania.
Kampuni hizo 38 kutoka Korea Kusini zitaungana na kampuni nyengine 50 za Tanzania ili kufanya uwekezaji wa ubia katika maji, miundombinu, mafuta, gesi na madini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri ndie ameyaeleza hayo.
Katika ziara yake ya kihistoria nchini Korea Kusini, Rais Dkt. Samia aliibua fursa za kiuchumi za Tanzania katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nishati ambayo wawekezaji wa Korea Kusini wangeweza kuingiza mitaji yao kupitia ubia na wawekezaji wa ndani.
#KAZIINAONGEA
0 Comments