HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAGOMBEA CHADEMA MBEZI WAREJESHA FOMU KWA KISHINDO



Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Makabe Kata ya Mbezi Mkoa wa Dar es salaam Geofrey Wilson amerejesha fomu yake leo katika ofisi ya Serikali ya Mtaa huo akisubiri uteuzi na siku ya kuanza Kampeni akisema ameridhishwa na mchakato ikiwemo kupokelewa vizuri.

Kwa upande wake Mgombea wa Nafasi ya Ujumbe Mtaa wa Makabe Kata ya Mbezi Mkoa wa Dar es salaam Magala Mussa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu ya nafasi ya ujumbe katika Mtaa huo akizungumzia hali halisi ya majina ya wananchi waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Viongozi wa Mitaa.

Mussa anasema wamebaini zaidi ya majina 500 yameongezwa na yameandikwa majina mawili badala ya matatu kwa mtu mmoja.



 

Post a Comment

0 Comments