HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA DKT SAMIA YAIKABIDHI TMA RADA MBILI


Na Mwandishi Wetu,

Ili kuhakikisha Mamlaka  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inafanya kazi zake kwa ufanisi, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu imekabidhi  rada mbili za hali ya hewa zilizopo Mwanza na Dar es salaam.

Rada hizo awali zilikuwa zinafanyiwa uboreshaji na kampuni ya Enterprises Electronic Corporation (EEC) kutoka Alabama nchini Marekani.

Serikali imegharamia maboresho hayo kupitia bajeti ya maendeleo yaliyolenga kuboresha ufanisi wa rada hizo zilizokwisha tumika kwa zaidi ya miaka 10 kwa kutoa vifaa vyenye teknolojia yenye software ya kizamani (edge 5) na kufunga ya kisasa (edge 6) ili kupata picha nzuri itakayoweza kutafsiriwa kiurahisi.

Maboresho hayo ni muhimu kwani yatawezesha kuendana na teknolojia inayotumika katika rada nyingine za hali ya hewa zilizofungwa hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Mbeya na Kigoma na hivyo kutumika katika mfumo jumuishi wa rada (MOZAIC)

Serikali imeendelea na  uboreshaji wa miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo ununuaji na ufungwaji wa rada tatu za hali ya hewa katika mikoa ya Mtwara, Kigoma na Mbeya na kufanya kuwa na jumla ya rada tano mpaka sasa ikiwa ni matazamio ya kufikia mtandao wa rada saba hapa nchini.

Rada hizi zina uwezo wa kufuatilia matukio ya hali ya kwa umbali wa nusu kipenyo cha zaidi ya Kilomita 250.

#KAZI INAONGEA

Post a Comment

0 Comments