HEADLINES

6/recent/ticker-posts

KAMATI YATOA MIEZI MIWILI KUKAMILIKA KWA JENGO TUME YA MADINI


Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.

Mwenyeti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt.David Mathayo David amemuelekeza mkandarasi wa ujenzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya Tume ya Madini kuhakikisha katika kipindi cha miezi miwili ijayo anakabidhi jengo kwa kamati.

Ameyabainishwa hayo leo Oktoba 18, 2024 katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya jengo iliyofanywa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi.


Dkt. Mathayo amesema kuwa, kwa kipindi kirefu watumishi wa Tume ya Madini wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kutokana ufinyu wa ofisi, hivyo kupelekea kushuka kwa utendaji kazi.

Aidha,Dkt.Mathayo amemtaka mkandarasi kuhakikisha katika kupindi cha miezi miwili ijayo anakabidhi jengo kwa Kamati ya Bunge likiwa limekamilika kwa asilimia 100 ili watumishi wote wa Tume ya Madini waweze kukaa sehemu moja ambapo itapelekea kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi wakazi tofauti na ilivyo sasa.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini, Dkt.Steven Kiruswa ameipongeza Kamati ya Bunge Nishati na Madini kwa ushirikiano mzuri inayoonesha pamoja na kutoa ushauri mzuri unaopelekea kuendeleza sekta ya madini katika kufuatilia na kukamilisha miradi yake kulingana na maelekezo ya kamati.

Naye, Kaimu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema, lengo la mradi huo ni kukamilika kwa jengo la ghorofa tatu ambapo ulitakiwa kukamilika na kukabidhiwa Oktoba 22, 2024 tofauti na ilivyo sasa.

Awali, akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi, Msanifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Vilumba Sanga amesema kuwa, hadi sasa mradi umefikia asilimia 93 katika maeneo mbalimbali ya jengo ikiwa pamoja na ufungaji wa miundombinu ya umeme, maji, dari, sakafu na uwekaji wa marumaru za sakafu na ukuta.

Mhandisi Sanga ameeleza kuwa, sehemu zinazoendelea na ujenzi ni pamoja na ujenzi wa uzio, ufungaji wa madirisha na upigaji rangi nje na ndani

Post a Comment

0 Comments