HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SASA KUPATIKANA WILAYANI MWANGA


 Na Mwandishi Wetu,
MWANGA,KILIMANJARO

Wanachi wa Halmashauri ya Wilya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro sasa kusogezewa huduma za Afya za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo huduma za upimaji wa kansa ya matiti kwa akina mama pamoja na Ultrasound kwa ajili ya kina mama wajawazito. 

Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 7, 2024 alipotembelea na kukagua  ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga unaotekelezwa kwa fedha za Serikali ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani Kilimanjaro. 
"Kwa sasa mgonjwa akitakiwa kupata huduma za X-Ray anakwenda Hospitali ya Mawezi au KCMC ambapo ni urefi wa Kilometa zaidi ya 50, lakini kwa sasa huduma hizo zitapatika katika Wilaya ya Mwanga zilizoletwa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
"Huduma hizi zitasaidia kuokoa gharama za wananchi wetu wa Mwanga kwenda kutunza mgonjwa wao mbali, zitasaidia kuokoa uchumi wetu maana mtu badala ya kuwaza mambo ya kuongeza uchumi atawaza mgonjwa yupo KCMC, Rais wetu amesema hapana inatosha, hayo yote yafanyike wapi? Hapahapa Mwanga." Amesema Waziri Mhagama 

 

Aidha, Waziri Mhagama amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni Mbili za mradi wa ujenzi wa Hositali hiyo ya Wilaya ya Mwanga pamoja na Milioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyotumika katika Hospitali hiyo. 

Amesema, miongoni mwa vifaaa vitakavyo nunuliwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na mashine ya kupima kansa ya matiti kwa akina mama, Ultrasound kwa ajili ya kina mama wajawazito pamoja na dawa ambao ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
"Nimeingia pale kwenye jengo la mionzi, nimekuta digital X-Ray ambayo ni toleo la kisasa kabisa, inauwezo wa kugeuza mwili wa mgonjwa pamoja na kupiga picha kwa ajili ya uchunguzi, haya mlikua mnayaona wapi ndugu zangu?." Amesema Waziri Mhagama
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha inatoa tiba sahihi kwa wakati sahihi, kwa mahitaji sahihi kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga." Amesisitiza Waziri Mhagama

 

Post a Comment

0 Comments