Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.
Polisi Tanzania limewakamata Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti Msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio lilifanyika Swaswa Dodoma mwezi May 2024.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema
“Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson”
“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani,
kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani”
“Watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza taarifa za ongo mitandaoni zinazosema RIP Binti aliyebakwa na kulawitiwa akutwa amefariki”
“Taarifa nyingine ya uongo inasema Mama wa binti huyo amedondoka na kufariki Watuhumia wawili wamekamata huko Arusha na wawili Mkoani Dar es salaam ambao majina yao ni Amos Lwiza, Adam Dongo, Venance Mallya na Isack Elias
Imetolewa na David Misime
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Dodoma, Tanzania.
0 Comments