Na AMEDEUS SOMI.
DODOMA.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema mikataba yenye thamani ya zaidi ya Trillioni 3 na Billioni mia saba ya Watanzania wazawa imesajiliwa na kusiriki katika ujenzi wa mradi wa Treni ya Kisasa ya SGR (Standard Gauge Railway).
Akizungumza Jijini Dodoma katoka uziduzi wa Mradi huo mkubwa nchini Kadogosa amesema mbali na ushirikishwaji wa Watznaznia katika mradi huo mkubwa pia ajira zaidi ya elfu thelathini zimetolewa mishahara iliyolipwa mpaka sasa kukamilika kwa mradi huo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni Billioni 358.4 na zimeenda kwa Watanzania waliofanya kazi katika mradi huo ajira zisizo rasmi zaidi ya laki moja na nusu
”Katika kusaini makubaliano ya mradi huu tulipendekeza wafanyakazi 80% watoke nje na 20% ndani lakini jumla 50% wametoka ndani, asilimia 92 ya wafanyakazi wote walitoka Tanzania”.
Kwa upande wa Reli na gharama za mradi Mhandisi Kadogosa ameendelea kusema kuwa kwa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma imegharimu kiasi Dola za marekani millioni 10 sawa na Shilingi Trillioni 25 ambapo ni jumla ya Kilomita 722 kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora, Singida na itakua na uwezo wa kubeba uzito wa tani elfu kumi ambayo ni sawa na malori 500 kwa mkupuo.
“Kwa upande wa Minara ipo 51 ambayo ni mingi kuliko ya Kampuni ya Simu ya Vodacom, tumetandaza Fiber 539 za mawasiliano ya intanet kwa ajili ya kuongozea treni lakini pia zipo Transmission Line kwa ajili ya uendeshaji wa reli tu ambayo haiingiliani na mtu yoyote ambayo imeunganishwa kwenye source ya umeme wa nchi nzima.
Mbali na ujenzi Shirika la Reli linatekeleza manunuzi ya vitendea kazi ikiwemo vichwa vya umeme 19 mabehewa 89, treni za kisasa seti 10, mabehewa ya mizigo 1430 mwishoni mwa mwaka huu yatakuja mengine 250.
Nyinginezo
Mpaka sasa tayari vichwa
vyote 17 vya Treni vimeshapokelewa
wamepokea mabehewa 65, Treni za Mchongoko 3 na wanaendelea kufanyia majaribio
na kufikia mwezi Septemba moja itaanza
kufanyiwa majaribio.
Fursa za ajira
Jumla ya wahudumu na wafanyakazi kutoka katika sekta binafsi
2460 wanashiriki na wanaendelea na ujenzi wa mradi huo, katika ujenzi huu mradi
umeshatoa ajira Zaidi ya elfu 30 na tayari imelipwa mishahara Billioni 358.4
kwa wafanyakazi wa Kitanzania.
Mpaka sasa tayari zimetoka ajira laki moja na hamsini kwa
wakandarasi na wataalamu wenye ujuzi na weledi wa hali ya juu.
Kadogosa amemaliza kwa kusema Ujenzi wa Majengo ya Stesheni za Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma umesanifiwa kwa kuzingatia uthamani wa vitu vilivyopo nchini.
Jengo la Dar es Salaam limefata sanifu ya Madini ya Tanzanite
ambayo duniani yanaptikana Tanzania pekee, Jengo la Stesheni ya Morogoro
limesanifiwa kwa kuzingatia safu ya milima ya Uluguru inayopatikana Mkoani
Morogoro na kwa Dodoma Jengo la Stesheni limezingatia Mawe yanayopatikana
katika Mkoa huo.
Kuhusu suala la abiria kutotakiwa kubeba mizigo mikubwa na
vitu vingine Kadogosa amesema kuwa kwa abiria watakaopanda daraja la Biashara
watatakiwa kubeba mizigo isiyozidi uzito wa Kilo 30 huku wa daraja la Juu
isizidi kilo 20.
Kwa kipindi hiki cha uzinduzi wa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro (tarehe 28 Julai) ni abiria 160,000 mapato Billioni 2.4 Kipande cha Dar es Salaam-Dodoma (tarehe 25-28 Julai) wamesafirisha abiria wamesafirisha abiria elfu 28,600 na kupata Millioni 744 na kwa ujumla mpaka sasa wamesafirisha abiria 188,00 hivyo kwa siku wanatumia abiria zaidi ya elfu saba
Changamoto
Ugonjwa wa Uviko na
mvua za vipindi vimetajwa kama vitu vilivyokwamisha kusuasua kwa mradi
huu mkubwa kuliko yote nchini Tanzania.
Mwisho Kadogosa akasema ataendelea kufaya kazi kwa utii na kusimamia kwa weledi mradi wa SGR akiwaasa Watanzania kuipenda reli yetu kwa sababu ni mali yetu kwa sababu reli hii itadumu kwa miaka 100, Kaulimbiu ya TRC ikiwa ni
“Twendeni tukapande treni yetu tuitunze”
Pia unaweza kutazama
0 Comments