HEADLINES

6/recent/ticker-posts

KASEKENYA ARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA ITEMBE

Na Mwandishi Wetu,

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya ameelezea kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Itembe mkoani Simiyu na kusisitiza likamilike kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 150 liko katika barabara ya Maswa-Meatu-Sibiti hadi Karatu inayounganisha kwa njia fupi mikoa ya Kanda ya ziwa na Kaskazini ambapo kukamilika kwake kutaleta tija kwa sekta ya usafirishaji, uzalishaji na utalii kwa wakazi wa mikoa hiyo.
"Kazi yenu ni nzuri mko asilimia 80 hakikisheni kasi yenu inaendana na ubora ili Serikali izidi kuwaamini na kuwapa miradi mingi wakandarasi wazawa", amesema Naibu Waziri Kasekenya.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS),Mkoa wa Simiyu Eng. Boniface Mkumbo amesema daraja hilo linalojengwa na mkandarasi mzawa Roctronic Ltd  pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa KM 2 litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 9.4 litakapokamilika.

Amesema katika kuhakikisha barabara hiyo ya inaimarika na kupitika wakati wote wa mwaka maandalizi ya kujenga madaraja ya Chobe mita 100 na Lyusa mita 75 yako katika hatua za mwisho.

Muonekano wa daraja la Itembe mkoani Simiyu ambalo ujenzi wake unaendelea






Post a Comment

0 Comments